Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
BAADA ya hivi karibuni kufungiwa video ya wimbo wake, staa wa muziki na filamu Bongo, Snura Mushi amesema ameendelea kuandamwa na majanga ambapo hivi karibuni alipata msiba wa babu yake huku mdogo wake akipata ajali.
Akizungumza kwa huzuni, Snura alisema mwaka huu umekuwa wa majanga kwake kwani babu yake huyo alimlea na kushika nafasi ya baba yake tangu alipozaliwa hadi kufikia utu uzima.
“Ukweli nimeumia sana na mwaka huu umekuwa ni wa 

majanga kwangu kwani babu yangu huyo nilikuwa namuita baba kwa sababu yeye ndiye aliyenilea mpaka nikafikia umri huu nilionao, mdogo wangu naye alipata ajali mbaya yuko hoi hospitali, utumbo ulitoka nje na kwenda kufanyiwa oparesheni, nimechanganyikiwa,” alisema Snura.
>>>>>>>GPL

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top