
Mkali wa mbio za magari duniani ambazo hujulikana kama Formula One “F1″, Michael Schumacher ,44,kutoka Ujerumani bado hajaweza kupata nafuu ya kuamka kutoka kwenye hali ya “Coma” baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye sehemu ya kichwa baada ya kupata ajali ya kuanguka na kujigonga sehemu hiyo nchini Ufaransa alipokuwa akifurahia mchezo wa kuteleza kwenye barafu (Skiing) mnamo Disemba 29, 2013
Kupitia gazeti la kila wiki la Ujerumani liitwalo Focus, limeripoti kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Schumacher kuwepo kwenye hali hiyo ya “Coma” kwa muda mrefu, au maneno mengine kwa maisha yote ambayo amebaki nayo baada ya kuongea na wataalam ambao wanahuska katika matibabu ya Michael.
Gazeti la Bild, nalo pia limeripoti habari hizo ambazo zinaonyesha hali ya mkali huyu wa mbio za F1 kuwa bado kwenye utata. Mpaka sasa yapata takribani siku 18, na kutokana na ukimya mwingi kutoka kwa timu ya madaktari wanaomtibu mjini Grenoble, nchini Ufaransa kumefanya hofu izidi kupanda kwa wapenzi wa mchezo huu.
Kuwa kwenye “Coma” inamaanisha, ukosefu wa hewa ya kutosha ya Oxygen kwenye ubongo, hivyo kupelekea ubongo kufanya kazi chini ya uwezo wake. “Brain injuries are among the most complicated injuries that can happen to the human body.”, alisema Professor Zieger amabye ni mmoja wa wataalam wanaosimamia matibabu kamilifu ya Schumacher.

Mke wa Michael Schumacher, Corrina pichani
Hofu hii imeendelea kuleta huzuni kwa watu wengi, ila familia ya mwanamichezo huyu, akiwemo mkewe Corrina na watoto wake wawili imeendelea kusimama imara katika kipindi hiki kigumu ambacho wanapitia.

Mashabiki wa F1 wakiwa wameshika bendera zinazoonyesha timu ya Ferrari nje ya hospitali aliyolazwa Schumacher
Source: Daily Mail
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment