Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
BAADA ya kuzagaa kwa habari kuwa viongozi wa kamati ya uchaguzi wa Klabu ya Bongo Movie wamepewa  rushwa, Mayasa Mrisho ‘Maya’ ameibuka na kukanusha taarifa hizo.

Mayasa Mrisho ‘Maya’.
Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar na kumtangaza Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ kushinda nafasi ya uenyekiti, baadhi ya wasanii waliibua minong’ono kuwa kamati ya uchaguzi ‘ilipozwa’ ili kupindisha matokeo.
“Hatukuchukua rushwa kutoka kwa mtu yeyote, uchanguzi ulikwenda vizuri na kila kitu kipo katika rekodi, anayetaka kuonyeshwa mfumo mzima wa kura atuone,” alisema Maya.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top