Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MSANII wa kike wa filamu Bongo Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefunguka kwa kusema kuwa mwanaume sahihi kwake na anayestahili kumuoa ni Rashid Mizengwe ‘Kingwendu’ kwa kusema anaamini ndiye anaweza kuwa mwaminifu na kuishi naye kwa raha tofauti na mwanaume mwingine yoyote endapo atapata bahati ya kuolewa naye.

“Unapofika umri fulani suala la kuolewa si mjadala bali ni lazima iwe hivyo lakini shida inakuja je utaolewa na mwanaume anayekujali, kuheshimu na kukupenda? Basi kwangu nataka kuolewa na mwanaume kama Kingwendu naamini nitakuwa na amani raha mstarehe, tofauti na kama nitapata sharobaro sina hakika kama atanijali,”anasema Rayuu kwa furaha.
 

Rayuu alisema alipokua akihojiwa na mwandishi  kuhusu mume gani bora kwake na angependa kuolewa naye na kuishi kama mke na mume, msanii alisema kuwa anahitaji mtu aliyetulia sambamba na umri wa makamo na mtu anayempenda sana kama awe mumewe ni msanii mwenzake Kingwendu au anayefanana nae.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top