Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Jeshi la Polisi wilayani Kibondo limewakamata watu wanne kwa kosa la kutaka kuvuruga mkutano wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa unaoendelea muda huu katika kata ya Mabamba wilayani Kibondo

Mwandishi wa Redio Kwizera Fm James Jovin amesema kuwa watu hao walikuwa na mabango yenye maneno yanayoonesha kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya CHADEMA ya kuwavua madaraka Zitto Kabwe na wenzake, lakini hata hivyo wameelekezwa sehemu ya kukaa ili mabango yao yaweze kusomwa vizuri na Dk Slaa, wamekaidi malelekezo hayo ambapo imebidi Dk Slaa aliagize jeshi la Polisi kuwakamata watu hao kwani mkutano huo ni kwa mujibu wa sheria

Watu hao ambao majina yao hayakujilikana papo hapo wamepelekwa kituo cha Polisi na Dk Slaa amemuagiza Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kibondo kufuatilia kesi hiyo kwa ukaribu

Source;JAMES JOVIN, REDIO KWIZERA

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top