
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa nchini Sudan
umesema kuwa utatumia ndege za upelelezi kujaribu kuhakikisha idadi ya
vijana walioripotiwa kuandamana kwenda kwenye mji wa Bor.
Serikali ya Sudan Kusini ilisema siku ya
jumamosi kuwa kulikuwa na maelfu ya vijana ambao ni wafuasi wa kiongozi
wa waasi Riek Machar.
Lakini msemaji wa waasi amesema kulikuwa na
askari wa kawaida ambao walikuwa wakirejea serikalini. Msimamizi wa
mazungumzo kutoka Afrika amewapa Bwana Machar na Rais wa Sudan Kusini,
Salva Kiir hadi Decemba 31 wawe wameanza mazungumzo.
Tayari maelfu ya raia wanatafuta hifadhi ya
ukimbizi katika kambi za Umoja wa Mataifa huku wanajeshi zaidi wa
kuongeza nguvu wa Umoja wa Mataifa wakiwa wamewasili nchini humo kwa
ajili ya kuimarisha usalama wa raia.
chanzo:bbc
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment