
Kigoma/Singida.Polisi mkoani Kigoma, imemshauri, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa kusitisha ziara zake mkoani Kigoma kwa sababu za kiusalama.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Zedekia
Makunja alisema jana: “Ni ushauri tu tunatoa kwa Dk Slaa kwamba anaweza
kuahirisha kutokana na hali ilivyo hapa.” Hata hivyo, Kamanda Makunja
alisema pamoja na yote hayo bado Polisi mkoani, Kigoma imejipanga imara
kukabiliana na vurugu zozote zinazoweza kutokea katika ziara hiyo.
Lakini Dk Slaa alipoulizwa kuhusu ushauri huo
alisema hawezi kufuta ziara hiyo na kusema hahofii chochote. Alisema na
alishafahamu siku nyingi kuwa hayo yanayotokea. Juzi, vijana mbalimbali
waliandamana kwa pikipiki na wengine wakitembea kwa mguu huku wakiwa na
mabango kupinga ziara ya Dk Slaa Kigoma. Anatarajiwa kuwasili Kigoma
Kaskazini keshokutwa.
Hatua hiyo ya kupinga ziara hiyo, imetokana na
Kamati Kuu ya Chadema kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa
Chadema, Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Wakizungumza baada ya maandamano yao yaliyoanzia
Kijiji cha Mwandiga kilichopo Kigoma Kaskazini hadi Uwanja wa Mwanga
Center, Kigoma, vijana hao walisema kundi hilo halimuungi mkono Dk Slaa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema katika Kijiji
cha Mwandiga, Mtoro Mvunye alisema: “Tumetoa wito kwa Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma, Luteni Kanali Issa Machibya na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma
(RPC) Fraser Kashai kusitisha ziara hiyo mara moja.”
Akizungumza baada ya kupokea maandamano hayo juzi,
Mvunye alisema hawataki kumwona Dk Slaa akifika katika Kijiji cha
Mwandiga, Ujiji na Mwanga.
“Kwanza nampongeza Mkuu wa Mkoa na RPC kwa
kusimamia vizuri maendeleo ya Kigoma, lakini nataka niwaeleze kwamba
endapo hawatachukua hatua ya kumzuia Dk Slaa kuja hapa Kigoma, hawa watu
wanatudharau sana sisi wa Kaskazini,” alisema Mvunye.
Alitoa wito kwa wanachama wa Chadema kutowapigia
kura kuwachagua viongozi wote wa mikoa na majimbo walioonyesha
kutomuunga mkono Zitto katika sakata hilo ambalo limesababisha
mgawanyiko kwa baadhi ya mikoa.
Mjini Singida, Baraza la Uongozi mkoani Singida,
limemtaka aliyekuwa Mwenyekiti Chadema Mkoa huo, Wilfred Kitundu kuomba
radhi ndani ya siku 14 kutokana na kutoa taarifa ya uongo, uzushi na
upotoshaji mkubwa wakati akitangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo. Taarifa
ya Baraza la Uongozi ilisema asipotekeleza agizo hilo, atavuliwa
uanachama. Akisoma taarifa hiyo, Kaimu Mwenyekiti, Shaaban Limu alisema
tuhuma zilizotolewa na Kitundu kuwa uamuzi uliotolewa na Kamati Kuu ya
kuwavua uongozi kina Zitto na wenzake ni za kipuuzi ni zake binafsi na
si za Chadema.
Vurugu zavunja mkutano wa Dk Slaa
Vurugu kubwa zilizuka jana na kusababisha mkutano
wa Dk Wilbrod Slaa uliokuwa ukifanyika kwenye Uwanja wa Kigalamo, Kasulu
kuvunjika. kwa habari zaidi BOFYA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment