Kamanda
wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Peter Ouma akiangalia Lori aina ya Isuzu
lenye nambari za Usajili T829 AHH mara baada ya kuanguka na kusababisha
vifoo vya watu wanne na majeruhi zaidi ya 30 katika ajali iliyotokea
Tarafa ya Ilolangulu wakati lilipokuwa likienda mnadani huku likiwa
limebeba wafanyabiashara wa mitumba pamoja na mizigo mbalimbali.
Tairi la Lori hilo ambalo lilikuwa bovu lilipasuka na kusababisha ajali hiyo mbaya.
Dereva wa Lori hilo Isuzu Bw.Ally Athuman ambaye alikutwa eneo la ajali hiyo mbaya
Baadhi
ya wananchi waliofika eneo la ajali wakishuhudia Maiti zilizokuwa
zimekusanywa kwenye gari la Polisi muda mfupi mara baada ya ajali
kutokea.
Madaktari
chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa ya Kitete mkoani
Tabora wakijaribu kuandika majina ya watu waliopoteza maisha na wale
waliojeruhiwa.
Kikosi
maalumu cha huduma ya kuokoa afya ya majeruhi katika hospitali ya
Kitete ambacho kilichukua hatua za haraka na makusudi kushughulikia
majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo.
Idadi
kubwa ya watu walivunjika miguu na mikono mbali na wale waliopoteza
maisha ambao majeraha makubwa walipasuka vichwa na kuumia vifuani.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment