STORI
kuhusu maisha ya mama mzazi wa staa wa komedi Bongo, marehemu Husein
Mkiety ‘Sharo Milionea’, baada ya kifo cha mwanaye huyo imemliza Rich
Mavoko ambaye alikwenda kumtembelea nyumbani kwake kijijini Lusanga,
Muheza mkoani Tanga.
Rich Mavoko akifuta machozi alipomtembelea Mama Sharo Milionea.“Mama alifurahi sana kuniona. Tulizungumza mengi lakini niliguswa sana na matatizo aliyonayo mama yetu. Mama anasema, mali nyingi za marehemu mwanaye, amekuwa akizisikia tu lakini hajapewa.
Mavoko na Mama Sharo wakiwa katika kaburi la Marehemu Sharo Milionea.Unajua marehemu alikuwa akimsadia sana mama yake, ndiyo lilikuwa tegemeo lake kubwa. Ameondoka na kumuacha akiwa hana la kufanya, mbaya zaidi hata mali zake ambazo zingepaswa kumsaidia kipindi hiki, wajanja wamezidhulumu.
“Dunia haina usawa kabisa. Kiukweli inatia huruma sana. Nawasihi wasanii wenzangu na wadau wa sanaa, inatakiwa tukumbuke wenzetu waliotangulia tena kwa kuwaenzi kwa kila njia.
Marehemu Sharo Milionea enzi za uhai wake.
Kuna vitu vinauma sana amenieleza tangu kifo cha mwanaye haki zake
nyingi hajui zilipo. Tuungane wasanii tuwasaidie wazazi wa wasanii
wanaotangulia mbele za haki,” alisema Mavoko.Credit: GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment