wachezaji wa liverpool wakishangilia baada ya kufunga goli mojawapo kwenye mchezo huu.
Baada ya jana man city kumshushia kipigo Arsenal cha mbwa
mwizi leo jioni ilikuwa siku nzuri kwa timu ya Liverpool pale walipo ishushia
kipigo cha hatari sana huku luis suarez akitupia magoli mawili ktika mchezo huo
uliochezwa kwenye uwanja wa white hart line .
Iliwachukua dakika kumi na nane pale mshambuliaji wao hatari
raia wa urugay luis suarez alipoipatia goli la kwanza kweny mchezo huo na 84’
suarez akaifungia goli la nne, pia atika dakika ya 40 kiungo Henderson
aliipatia bao la pili timu yake , dakika ya 75 beki wa kulia wa Liverpool alipokea
pasi mulua kutoka kwa suarez na kutupia mpira nyavuni ,winga stering dakika ya
89 aliipatia Liverpool goli na kuhitimisha ushindi wa leo wa magoli matano kwa
bila na Liverpool kuwa nyuma ya Arsenalkwa point 2 huku Liverpool wakiwa na
34 juu ya celsea na man city.
Ilikuwa ni siku nzuri sana kwa mshambuliaji wa timu hiyo
luis suarez alipofunga magoli mawili na kutoa pasi mbili za magoli .
Kiungo wa tottenham
paulinho alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea Luis suarez mchezo
mbaya katika dakika ya 63 ya mchezo na timu yake kumaliz ikiwa pungufu ya
mchezaji mmoja.
Mechi iliyotangulia kabla ya Liverpool Manchester united
bada ya kupoteza mechi mbili mfululizo leo wamepata ushindi kwa kuifunga aston
villa magoli 3 kwa bila.
Mshambuliji wao Welbeck katika dakika ya 15 na 18 aliipatia
timu yake maoli mawili ya araka haraka na kuiweka Manchester kwenye nafasi
nzuri ya kuhukua point tatu kwnye mechi ya leo.
Ilikuwa ni siku nzuri pale kiungo mkabaj wa timu hiyo Fletcher
aliporejea kikosini baada ya kukaa nje kwa kipindi kirefu .
Iliwachukua dakika ya 52 kiungo wa timu hiyo cleverly alipotupia
goli ta 3 na la mwisho kwenye mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa villa
park. swansea na norwich city zimetoka sare ya goli 1 kwa 1.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment