Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
mandela 
Mazishi ya mzee Nelson Mandela yamefanyika  muda huu katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape na kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa huyu wa Afrika mzee Nelson Mandela.

Idadi ya Takribani watu 4,500 wakiwemo wageni wa kimataifa wamehudhuria mazishi hayo yaliyofanyika katika kijiji chake ,mazishi yake yamekuwa ya  mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.

Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale huku wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa.
1483139_563742170368160_40127197_n 
Moja kati ya mataifa yaliyopata heshima ya kuongea mbele ya viongozi mbalimbali duniani ni Rais wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Eneo analozikwa mzee Nelson Mandela ni sehemu ya  makaburi yaliyo kwenye shamba kubwa la familia ya Mandela lililoko katika kijiji cha Qunu lililojengwa mara baada ya kuachiliwa kutoka jela mwaka 1990, katika eneo lenye nyasi za kijani , na milima ya Cape ya mashariki.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top