Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Joyce Kiria akiwa amembeba mtoto wa Emma.
Joyce Kiria akizungumza na Emma.
Vitendo vya ubakaji vimeendelea kuumiza akili za wapigania haki na ustawi wa wanawake nchini Tanzania kwa muda mrefu sasa. Miongoni mwa kesi hizi zimehusisha wasichana wadogo wenye malengo makubwa katika maisha yao, lakini kutokana na mfumo uliopo, jamii hushindwa kutoa msaada kwa wahanga wa matukio hayo ili wafanikishe malengo yao.

Emma Roberts ni binti mwanafunzi aliyekumbwa na mkasa wa kufukuzwa shule kutokana na ujauzito alioupata baada ya kubakwa. Kupitia kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na East Africa Television kila Jumanne saa tatu usiku, binti Emma anaelezea tamaa yake ya kufanya mtihani mwezi Novemba, kwa kuwa anaamini kuwa elimu itamsaidia yeye na mwanaye ambaye atalelewa bila kuwa na baba. Kitendo cha kufukuzwa shule kwa tukio kama hili kumemuathiri kwa kiasi kikubwa, na sasa ana hofu ya kutimia kwa malengo yake hapo baadae.


Kumnyima fursa hiyo ya kuendeleza elimu yake ni kutengeneza taifa lenye wanawake wasio elimu na masikini. Kitendo kilichomkuta Emma, kinaweza kuwakuta wasichana wengi nchini Tanzania. Kuna wale waliojitokeza hadharani, lakini vipi kuhusu wale walioamua kukaa kimya?

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top