Viongozi Wakuu wa vyama
vya siasa nchini Tanzania, NCCR-Mageuzi, CHADEMA na CUF wametangaza
kusitisha mpango wa maandamano uliokuwa umepangwa kufanyika siku ya
Alhamisi, Oktoba 10, 2013 katika maeneo ya mikoa ya Unguja, Dar es
Salaam, Mbeya, Kigoma, Dodoma, Tanga, Mwanza na Arusha kwa lengo la
kudai upatikanaji wa muafaka wa mchakato wa Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba yatakayowezesha kuundwa kwa Katiba Mpya inayokubalika na
wananchi.
Mwenyekiti wa CUF akizungumza kwa niaba ya viongozi
wenzake katika ofisi za Makao Makuu ya NCCR-Mageuzi jijini Dar es Salam,
Profesa Ibrahim Lipumba amesema sababu kubwa ya kusitisha mikutano
iliyopangwa inatokana na kuitambua nia ya Rais
Kikwete aliyoionesha katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, ambapo
alibainisha wazi kuwa atakutana na viongozi wa vyama hivyo kuzungumzia
suala hilo la Muswada wa Katiba.
Kutokana na nia hiyo, alisema vyama hivyo havina budi kusubiri mazungumzo na Rais Kikete yatakayotoa dira ya kitakachoendelea katika lengo la kupata katiba shirikishi na inayokubalika na raia wengi.
“Tumesikia kupitia vyombo vya habari ambavyo navyo vimenukuu taarifa kutoka Ikulu, inayobainisha kuwa Rais Jakaya Kikwete amepanga kukutana na viongozi wa upinzani kati ya Oktoba 13 na 15 ili kujadili na kupata muafaka wa suala hili la Katiba.
"Tunaamini kuwa taarifa hizi ni sahihi kabisa, hivyo tumeamua kusitisha maandamano yetu, yaliyolenga kushinikiza nguvu ya umma kuungana nasi katika kudai mchakato wa kuipata Katiba shirikishi, na kushinikiza Rais kutosaini kabisa muswada huo wa sheria kwa kuwa una upungufu,” alisema Profesa Lipumba.
Viongozi hao pia wamesema wapo tayari kusubiri kukutana na Rais katika tarehe itakayopangwa na kuafikiwa.
“Pamoja na kuahirisha maandamano haya, tunapendekeza huo mkutano ulioahidiwa na Rais, ufanyike mapema ili mchakato wa Katiba unaosuasua kwa sasa uendelee kwa ufanisi,” alisema Lipumba.
Ikiwa mazungumzo hayo hayatafanikiwa, viongozi hao wameahidi kurejesha ratiba ya maandamano na mikutano.
Mwenyekiti wa CUF akizungumza kwa niaba ya viongozi
wenzake katika ofisi za Makao Makuu ya NCCR-Mageuzi jijini Dar es Salam,
Profesa Ibrahim Lipumba amesema sababu kubwa ya kusitisha mikutano
iliyopangwa inatokana na kuitambua nia ya Rais
Kikwete aliyoionesha katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, ambapo
alibainisha wazi kuwa atakutana na viongozi wa vyama hivyo kuzungumzia
suala hilo la Muswada wa Katiba.Kutokana na nia hiyo, alisema vyama hivyo havina budi kusubiri mazungumzo na Rais Kikete yatakayotoa dira ya kitakachoendelea katika lengo la kupata katiba shirikishi na inayokubalika na raia wengi.
“Tumesikia kupitia vyombo vya habari ambavyo navyo vimenukuu taarifa kutoka Ikulu, inayobainisha kuwa Rais Jakaya Kikwete amepanga kukutana na viongozi wa upinzani kati ya Oktoba 13 na 15 ili kujadili na kupata muafaka wa suala hili la Katiba.
"Tunaamini kuwa taarifa hizi ni sahihi kabisa, hivyo tumeamua kusitisha maandamano yetu, yaliyolenga kushinikiza nguvu ya umma kuungana nasi katika kudai mchakato wa kuipata Katiba shirikishi, na kushinikiza Rais kutosaini kabisa muswada huo wa sheria kwa kuwa una upungufu,” alisema Profesa Lipumba.
Viongozi hao pia wamesema wapo tayari kusubiri kukutana na Rais katika tarehe itakayopangwa na kuafikiwa.
“Pamoja na kuahirisha maandamano haya, tunapendekeza huo mkutano ulioahidiwa na Rais, ufanyike mapema ili mchakato wa Katiba unaosuasua kwa sasa uendelee kwa ufanisi,” alisema Lipumba.
Ikiwa mazungumzo hayo hayatafanikiwa, viongozi hao wameahidi kurejesha ratiba ya maandamano na mikutano.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro

Post a Comment
Post a Comment