Hakuna aliye kamili katika dunia hii, hata Mungu anakusamehe kwa njia zako na matendo yako, si kweli kwamba wewe ni msafi sana hadi leo bado uko hai, bali Mungu ni mwenye huruma anakusamehe. Aidha unapaswa kufahamu kuwa kuna faida za kuoa mapema. Ndoa tamu bwana asikwambie mtu tena ni raha uipate ndoa ukiwa kijana, nyumba ujenge ukiwa kijana, gari ununue ukiwa kijana, siyo hadi unakuwa babu. Faida ni kujenga maisha mapema, kujipanga vizuri na kujenga familia. Ni furaha unapokuwa na watoto ambao ni kama wadogo zako. Kuzaa ujana ni raha zaidi, kuliko ukizaa ukiwa na zaidi ya miaka 35. Pia usiogope kuoa mapema kwamba eti utapitwa na mambo ya ujana si kweli, mambo ya kujinafasi bado yapo, yalikuwepo na yataendelea kuwepo na yanakuwa ni ya kiutu uzima zaidi, ni ya staha na heshima mbele, fujo fujo hakuna. Pia kuna tafiti za kisayansi zinaonyesha watu wanaopata watoto wakiwa na zaidi ya umri wa miaka 35, wanapata watoto wenye akili ndogo. Wenye hoja za kutokuwa na mpango kabisa wa kuoa, wana matatizo ya kisaikolojia na wanapaswa kuachana na fikra hizo mbaya kwamba kuoana ni kubaya. Ukizoea sana kuishi kisela au kubadili wanaume au wanawake kama nguo, mwishowe unakuwa huwezi tena kutulia, na ndiyo hao ambao baadhi yao wamekuwa wakiona hakuna haja tena ya kuoana. Kuna wanaoogopa kuoa au kuolewa wakiamini ni jela fulani hivi, kumbe hilo si la kweli. Ukweli ni kwamba ukiwa kwenye uhusiano na mkaelewana vizuri, mafanikio huwa makubwa. Katika maisha pia kuna suala la nyota, kwamba wapo watu ambao ukiwa nao ni kama kujitia mikosi, kuna mwingine ukiwa naye tu, unashangaa mambo yanakwenda safi, ni suala la kutafakari kwa makini suala la kuwa na mwenza ambaye ni wa kudumu na ambaye anatambulika kisheria na mbele ya Mungu.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment