Idadi ya wasanii wa bongo fleva wanaovuta majiko (kuoa) inazidi
kuongezeka, na safari hii aliyeiaga kambi ya ukapela ni hit maker wa
‘Kwaajili Yako’ Hussein Rashid maarufu kama Hussein Machozi ambaye
(August 28) amefunga pingu za maisha kimya kimya na Shu Yunus Omar raia
wa Kenya.
Kupitia kurasa zao za facebook wote wawili Hussein Machozi na mkewe Shu Omar wamebadilisha status zao kutoka ‘In a releationship’ na kuwa ‘Married’ huku mkewe akielezea furaha yake kuwa mke wa staa huyo kutoka Manyoni, Singida.


Hizi ni baadhi ya picha za chaguo la Machozi





Addicted Hit maker pia ni baba wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Zakia.
Hongera sana Hussein kwa kupiga hatua hiyo kubwa katika maisha
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment