Kwa mujibu wa TFF usajili umeshaanza na mikataba
ya wachezaji itaanza kupokelewa katikati ya mwezi huu kabla ya kuanza
kupitiwa na kamati husika kuangalia uhalali wake mwishoni mwa Julai.
Yanga, ambao msimu huu hawasajili wachezaji wengi
iliwasilisha mkataba wa Ngassa wiki iliyopita, lakini watendaji wa TFF
wakagoma kupokea kwa madai kwamba bado muda wake haujafika.
“Mikataba yote itaanza kupokewa Julai 15, kwa hiyo
tumewaambia Yanga kuwa wasubiri kwani muda wa kuleta mikataba bado,”
kilisema chanzo kutoka TFF.
Mabingwa hao wa Tanzania ambao walimsainisha
Ngassa mkataba wa miaka miwili walikuwa wakishinikiza mkataba huo ubaki
kwa shirikisho hilo ili kuepuka fitina zinazoweza kufanywa na Simba
ambao wamekuwa wakidai kwamba wana mkataba na Ngassa.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ambaye inadaiwa
ndiye aliyepeleka mkataba huo aligoma kutamka lolote alipoulizwa. Yanga
ipo kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa ziara ya mechi za kirafiki
kujiandaa na msimu mpya ikiwa imeambatana na Ngassa.
Kwa mujibu wa kanuni ya 35 ya Ligi Kuu Bara
inayohusu kipindi cha usajili kifungu cha “(2) Klabu zinawajibika
kutumia mikataba iliyotayarishwa na Shirikisho kuhamisha/kuazima na
kusajili wachezaji wake, mikataba mingine yote haitatambulika.
“(3) Kutangaza wachezaji ambao klabu inasitisha
mikataba yao, uhamisho na usajili wa wachezaji utafanywa na walimu wa
klabu katika kipindi kitakachotangazwa na TFF.”
mwanaspoti
mwanaspoti
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment