Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametoa kali ya mwaka baada ya kunaswa akiingia ‘supermarket’ akiwa ametinga taulo.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika mji wa Maryland nchini Marekani ambapo staa huyo amekwenda kwa ajili ya kufanya shoo kisha kupigwa picha hiyo na rafiki yake ambaye aliiweka mtandaoni ikimuonesha akiwa amefunga taulo kwenye matiti.
 

Mwandishi wetu alipomuuliza Shilole kulikoni kupitia mtandao wa Instagram, alifunguka:
 

“Huku watu wanaishi kizungu hakuna mtu anayeshughulika na maisha ya mwenzake kila mmoja anahangaika na mambo yake kwa hiyo siyo ajabu mimi kuvaa taulo na kwenda nalo supermarket, huku ni kawaida tu.”

GP

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top