Muingizaji wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa tano usiku wa Jumatano iliyopita kwenye hoteli hiyo iliyopo Kawe Beach, jijini Dar.
Akizungumza
na mwandishi wetu , meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa
nane mchana, Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa
ameongozana na marafiki zake wapatao kumi.
Meneja huyo akaendelea kusema, ilipofika saa tano usiku, Wema na marafiki zake walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo.
Aliongeza kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa makusudi huku meneja huyo akishuhudia.
Meneja akasema: Wakati wanaondoka, nilimfuata yule jamaa mpaka nje, nikamuuliza ni kwa nini amevunja glasi kwa makusudi, akanijibu kwa dharau huku akinitukana na kutishia kunipiga, akawa ananiuliza hiyo glasi ni shilingi ngapi kwani ?.
Aliongeza
kuwa swali lake kwa kijana huyo lilionesha kumkera sana Wema, kwani
alitoka kwenye gari na kuanza kumlamba vibao visivyo na idadi meneja
huyo huku akimpa maelekezo kwamba akashitaki popote na hawezi kufanywa
kitu kwani yeye ana nguvu kwenye nchi hii.
“Niliamua kupiga simu Kituo cha Polisi Kawe, wakaja kuangalia mazingira kisha nikaondoka nao kwenda kufungua kesi kituoni.”
TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2009, Wema alidakwa na
Polisi Kituo cha Magomeni na baadaye kupandishwa katika Mahakama ya
Kinondoni, Dar kwa Hakimu Emilius Mchalu kwa kosa la kuvunja kioo cha
gari la aliyekuwa staa wa filamu Bongo, Marehemu Steven Kanumba chenye
thamani ya shilingi milioni moja.
Hata hivyo, Kanumba aliamua
kuifuta kesi hiyo kwa sababu ya kutaka amani. Wakati huo Wema alikuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mjasiriamali aitwaye Jumbe Yusuf Jumbe.
ALIMTISHIA MAISHA BOB JUNIOR
Kama vile haitoshi, mwaka
2011, Wema huyohuyo alilikwaa soo jipya, akakamatwa na Polisi wa
Oysterbay na kufikishwa Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la
kumtusi na kumtishia maisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rahem Nanji ‘Bob
Junior’.
Katika kesi hiyo, Hakimu
Mariam Masamalo alimtia hatiani Wema na kumhukumu kwenda jela miezi
sita au faini ya shilingi elfu arobaini ambapo alilipa feha hizo. Wakati
huo, Wema alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamon
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment