Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mmoja kati ya watu mashuhuri duniani haswa katika ulimwengu wa vipindi maalumu vya mahojiano vya televisheni, Opra Winfrey yuko ziarani katika Mbuga ya Taifa ya Serengeti katika ziara yake binafsi.
kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mwanamke huyo mashuhuri ambaye ni mwanzilishi na mmiliki wa vipindi maarufu duniani vya Opra Winfrey Show, lakini pia maarufu katika filamu kadhaa ikiwemo ya hivi karibuni ya 'The Butler aliyoigiza kama Cloria Ganines, imeripotiwa atakuwepo Serengeti kwa wiki nzima kuanzia wikiendi iliyopita



“itakuwa ni ziara ya kibinafsi tu” alisema Paschal Shelutete alipohojiwa na chombo kimoja cha habari, ambaye ni Afisa Uhusiano wa TANAPA (Tanzania National Parks), ambayo inaendesha mbuga zote za taifa nchini.


Ziara yake hiyo pamoja na kuwa binafsi haitomzuia kukutana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ambaye pia yuko safarini kumpokea na kumkaribisha mgeni huyo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top