Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mchekeshaji mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo Amri Athuman ‘King Majuto’ ametamba kwa kujigamba kuwa yeye ndio msanii au mchekeshaji pekee asiyechuja katika tasnia ya filamu na vichekesho, King Majuto kayasema hayo wakati akihojiwa na wanahabari alipoulizwa kwanini anashiriki katika filamu nyingi tofauti na wachekeshaji wengine?

Unajua mimi ndio mwigizaji niyeyushuka katika uigizaji kwa miaka mingi, tulikuwepo wengi lakini wamepotea hata kunyanyua ni shida, lakini pia jambo lingine ambalo nimeliona ni nidhamu, kuna watu wanajisahau wakifanya vizuri katika michezo, mtu ataambiwa kuwa tunatakiwa katika Location saa fulani hatokuja kwa muda huo,”anasema King majuto.

Pia amedai kuwa amekuwa akiigiza na vijana wanaofanya vizuri katika filamu lakini anahisi kukosa mrithi wa kipaji chake zaidi ya mtoto wake Mohamed ambaye anafanya vizuri na ana nidhamu tofauti na wasanii kama Hemed hivi na wengine wenye kazi nyingi ambao kuna wakati usababisha hata kazi kukwama kwa wao kutofika kwa muda uliopangwa.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top