Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MUZIKI wa kizazi kipya ni moja ya fani iliyotoa ajira kwa vijana wengi nchini huku wengine wakiendesha maisha yao kupitia muziki huo.

Mnamo miaka ya 1999 kulikuwa na ongezeko la vipaji lukuki kwa baadhi ya vijana wengi huku wengi wao wakiingia katika fani hiyo ya muziki kwa ajili ya kujiajiri na kufikisha ujumbe kwa jamii.


Msanii Taikuni Ally 'Mchizi Mox' ni miongoni mwa vijana ambaye alijiunga na fani ya muziki wa kizazi kwa ajili ya kuendeleza kipaji chake pamoja na kuinua kipaji chake.


Mchizi Mox alianza safari yake ya muziki akiwa masomoni kwa kujiunga na bendi ya shule, kuimba pamoja wanafunzi wenzake, huku akiwa na ndoto ya msanii mkubwa nchini.


Mchizi Mox aliamini juhudi ndizo zitakazomfanikisha mafanikio yake, kutokana na hilo aliamua zaidi kujikita katika mambo ya sanaa hata kupiga ngoma mbalimbali alipokuwa masomoni.


Akielezea historia yake kwa ufupi msanii huyo aliweka wazi kuwa, aliamua kujiunga na na mambo ya sanaa ya muziki wa kizazi kipya huku akipata ushirikiano kutoka kwa wazazi wake.


Kabla ya kuunda kundi la Wateule, Mox aliweza kufanikiwa kutoa single iliyojulikana kwa jina la 'Watoto wa mitaani' nyimbo iliyobeba ujumbe na kuelimisha jamii juu ya kudhibiti na kupunguza watoto wa mitaani.


Aliweza kufanikiwa kurekodi nyimbo hiyo kwa msaada wa mama yake ambaye alimpa ushirikiano wa kwenda studio kurekodi ikiwemo kumlipia gharama zote za studio.


Baada ya muda Mox aliweza kunga'ra akiwa na wenzake Jafarray pamoja na Jaymoe kwa kushinda katika mashindano ya kuibua vipaji vya muziki ambapo waliteuliwa kuwa ni kundi bora la Hip Hop.


Hapo ndipo kundi la 'Wateule' lilipoanza katika studio ya bongo records, baada ya kufika katika studio hizo washindi hao kwa ajili ya kurekodi nyimbo ikiwa zawadi ya ushindi huo ndipo jina la wateule lilipozaliwa.


Msanii huyo alianza safari yake ya muziki mnamo 2000, pamoja na kuunda kundi hilo la wateule na kufanikiwa kutoa 'single' iliyokuwa inawatambulisha katika jamii.


Baada ya muda kidogo kundi hilo lilivunjika ambapo kila mmoja alianza kufanya kazi kwa mtindo wa pekee yake, hivyo Mox alibaki kwa muda bila ya kutoa nyimbo yoyote kwenye jamii hali hiyo ilimpa changamoto kwa mashabiki wake.


Baada ya kimya cha muda mrefu Mox aliendeleza kundi hilo la Wateule kwa kutoa nyimbo iliyojulikana kwa jina la 'Watu kibao' miaka 2001 ambapo nyimbo hiyo iliibua hisia kwa mashabiki walioisahau kundi la wateule.


Aliweza kufanya vyema katika mambo ya muziki huku ndoto zake ni kuendelea kuwa msanii mkubwa, aliweza kufanikisha malengo yake kwa kutoa single nyingine ambayo ilimtambulisha Mox katika suala zima la muziki.


Nyimbo ya 'Mambo vipi' ilikuwa ni jibu kwa Mox ambapo aliweza kuibua na kuteka hisia za mashabiki wake huku akiendelea kuongeza mashabiki lukuki kutokana na ujumbe pamoja na aina ya uimbaji wa nyimbo hiyo huku sauti yake ikiendelea kuwa mvuto ndani ya nyimbo.


Mambo vipi, ilimuongezea mashabiki lukuki huku, pamoja na kuongeza imani kwa wasanii wenzake huku baadhi yao wakiwa na kiu ya kushirikiana nao katika kazi ya muziki.


Mox anajivunia mvuto wa sauti yake ambayo imemfanya kumuongezea kufanya kazi na wasanii wengi huku baadhi yao wakiamini kuwa ubora wa sauti yake ndiyo inaweza kuboresha nyimbo anazoshirikishwa.


Mox ambaye amefanya kazi za kushirikishwa na wasanii wengi hapo mwanzo, sasa ameweka bayana msimamo wake wa kutofanya kazi za kushirikishwa kwani anaona hazina faida kwake.


Mox baada ya ukimya wa muda mrefu sasa anajipanga kurudi tena kwenye gemu kwa kuachia albamu yake ya pili ambayo ataipa jina la 'Goli la pili na mwisho wa mchezo' ikiwa ndio albamu yake ya mwisho huku albamu yake ya kwanza aliipa jina la 'Goli la kwanza'


Msanii huyo aliweka wazi kuwa hana mpango wa kuendelea kutoa albamu kwani albamu hizo hazilipi ila anayoitoa ni ya mwisho na kuendelea kubaki kutoa single

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top