Ndege ya kivita F-16
Marekani inaendelea na mpango wake wa kutoa ndege za
kivita kwa jeshi la Misri licha ya msukosuko wa kisiasa unaokumba nchi hiyo.
Hatua hii inajiri wakati Marekani ikiendelea kutathmini matukio ya wiki jana
ambapo jeshi lilimuondoa madarakani Rais Mohammed Morsi.
Msaada wa
kijeshi kwa Misri ungesitishwa endapo Marekani ingelitaja matukio ya wiki jana
kama mapinduzi ya kijeshi. Kundi la Muslim Brotherhood linalomuunga mkono Morsi
linasisitiza arejeshwe madarakani.
Wafuasi wake
wamekua wakiandamana karibu na kambi kuu ya jeshi ambapo anaaminika kuuzuiliwa.
Hapo Jumatatu,wafuasi wa Brotherhood 51 waliuawa kwa kupigwa risasi na jeshi
wakati wanakabiliano.
Utawala wa
mpito umesema kwamba Bw. Morsi anazuiliwa eneo salama na kwamba haki zake
zinazingatiwa. Maafisa wa Marekani wamesema ndege mpya za kivita aina ya F-16
zitawasilishwa katika wiki chache zijazo.
Mpango wa
kufadhili jeshi ulianza kutekelezwa mapema mwaka huu na jeshi linatarajia
kupokea ndege 20 za kivita. Msemaji wa ikulu ya Rais amesema Marekani
haitabadilisha mpango wa kufadhili jeshi la Misri, japo inaendelea kutathmini
kuhusu matukio ya kisiasa. Msaada wa kijeshi nchini Misri ambao hutolewa na
Marekani hufikia dola bilioni 1.3 kila mwaka.
Hapo Jumanne,
kibali cha kumkamata kiongozi wa Muslim Brotherhood Mohamed Badie kilitolewa
pamoja na wakuu wengine tisa wa kundi hilo. Viongiozi hao wamelaumiwa kwa
kuchochea ghasia mjini Cairo ambapo zaidi ya watu 50 waliuawa na mamia
kujeruhiwa.
Chanzo: BBC SwahiliFacebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment