Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au ya njano, ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya.
Ila  majimaji yanayotoka yakiwa  katika hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yakiwa yanatoa harufu mbaya na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis.

Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili.
Utokaji huo wa uchafu ni njia ya kuvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bakteria au fangasi wanaoleta magonjwa. Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano.
 Pia huwa na asidi ya lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi za Bartholin. Kwa kawaida, mwanamke hutoa kiasi cha gramu 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji wa uzazi na gramu 3 za ute mwepesi kila siku.
Kiwango hiki huweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi. Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika (kama ute wa yai la kuku) na kuna wakati huwa mzito kiasi na wenye rangi ya njano.
Ute huu ni wa kawaida na huwatoka wasichana au  wanawake wote baada ya kuvunja ungo.

SABABU ZA KUTOA UTE
Katika uchunguzi wa kitaalamu imegundulika kuwa kuna mambo mengi yanayosababisha mwanamke kutoa ute au majimaji yasiyo ya kawaida kwenye sehemu zake za siri.
 Maambukizi ya bakteria wanaosababisha magonjwa kama Trichomoniasis, Candidiasis, Kisonono au Gonorhear au uambukizo wa bakteria Candida albicans na Vaginosis husababisha mwanamke kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu mbaya.
Pia kukaa na pedi muda mrefu sana bila ya kubadilishwa wakati wa hedhi,  huweza kusababisha tatizo hili na kuwa mazalia mazuri ya bakteria wanaosababisha harufu mbaya.

DALILI
Wanawake wenye tatizo la Vaginosis huwa na dalili kubwa ya kutokwa na
uchafu usiyo wa kawaida  sehemu za siri. Uchafu huu huwa unatoa harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.



Tukasema kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au ya njano, ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya.
Ila majimaji yanayotoka yakiwa  katika hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yakiwa yanatoa harufu mbaya na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis.Tulieleza mengi na tukataja na sababu za kitaalamu kuwa imegundulika kwamba kuna sababu nyingi ambazo husababisha mwanamke kutoa ute au majimaji yasiyo ya kawaida kwenye sehemu zake za siri.
Leo tutaeleza dalili kisha tutaeleza vipimo na tiba ya maradhi haya ya kike katika jamii yetu.

DALILI
Wanawake wenye tatizo la Vaginosis huwa na dalili kubwa ya kutokwa na
uchafu usiyo wa kawaida  kutoka sehemu za siri. Uchafu huu huwa unatoa harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.
Wakati mwingine uchafu wenye rangi kama ya kijani hutoka,kuwashwa sana sehemu za siri, mgonjwa asipopatiwa tiba haraka husababisha vidonda sehemu za siri kwa sababu ya kujikuna kutokana na mwasho anaoupata.
 Kuna wakati mwingine  mwanamke anatokwa na ute uliochanganyikana na damu hata kama hayupo kwenye siku zake, hii ni dalili nyingine ya Vaginosis. Mgonjwa pia anaweza kusikia maumivu makali wakati wa tendo la ndoa, hali ambayo pia inaweza kusababishwa na kuingiwa kwa bakteria katika mji wa uzazi.
Bakteria hao huweza kusababisha siyo harufu tu, bali mgonjwa anaweza kutokwa na usaha sehemu hiyo ya siri.

MATIBABU
Tatizo hili hutibika hospitalini baada ya vipimo vya kitaalamu kuchukuliwa na mtaalamu mwenye uzoefu wa kutosha juu ya magonjwa ya wanawake. Daktari anaweza kumpa mgonjwa dawa za kupaka na dawa za kumeza ambazo huweza kumaliza tatizo hili.

USHAURI
Mara nyingi nashauri kuwa ni makosa kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari aliye na ujuzi wa magonjwa hayo na siyo kupewa dawa na wauzaji wa maduka ya dawa.
Nasema hivyo kwa sababu watu wengi wana kawaida kwenda kwenye duka la dawa na kupewa dawa na muuzaji bila kupimwa. Kumbuka unaweza kupewa dawa ambayo siyo ya ugonjwa wako.
Nawashauri pia wale wanawake wenye kawaida ya kutumia pafyumu au kuweka dawa sehemu za siri kwa lengo la kuzifanya kuwa ndogo, waache kufanya hivyo kwani madhara yake ni makubwa sana kiafya likiwemo hilo la kutoa harufu mbaya sehemu hizo na zinaweza kusababisha madhara makubwa katika njia ya uzazi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top