Msanii wa Commedy nchini na muimbaji wa
bongo fleva Kitale rais wa mateja, amekanusha taarifa zinazomuhusiha
na mali za Marehemu Sharo milionea.
Katika A/C yake ya BBM Kitale ameandika
"mama wa marehemu sharo Milionea ametoa malalamiko juu ya kutokabidhiwa baadhi ya mali za marehemu Sharo.
Waandishi bila kumuelewa mama, wao moja kwa moja wananihusisha na
mimi kuwa nahusika. Hii ni kwa watanzania wote, Marehemu Sharo
Milioneaaliacha gari aina ya Oper, naom,ba kuwaambia watanzania ile gari
haipo chini yangu, ile Gari ipo chini ya Muddy Suma, ambaye ni mwenye
gari aliyopata nayo ajali Sharo na mama yake Sharo kulalamika kwenye
vyombo vya habari ni sawa na ni haki yake kwa sababu mwenye Gari
aliahidi kusamehe, ila aliomba aachiwe mpaka atakaponunua gari nyingine.
Kinachoshangaza sasa ni mwaka unakwenda gari haijauzwa wala nini kwa
hiyo mama anahisi mimi na Mudy suma letu moja. Hapana mzazi wangu mimi
nipo pamoja na wewe, na watanzania wote naomba muelewe gari sinayo
mimi,. maana kila muandishi ananiandama mimi. Kitu ambacho mimi na
Sharo tulishea ni move tu. Gari anayo Mudy suma sababu yeye ndiyendiye
aliwezesha na kuhusu sofa anazo Mudy Suma"
Tutamtafuta Mudy Suma ili aweze kuthibitisha haya.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment