Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
clip_image001Klabu ya Ujerumani Borrusia Dortmund imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang toka klabu ya Ufaransa ya St Ettienne.

Aubameyang mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano ndani ya Dortmund na ujio wake huenda ukawa ishara ya mipango ya klabu hiyo kuwa mbioni kumuuza mshambuliaji wake raia wa Poland Robert Lewandowski ambaye amekuwa akisakwa na klabu za Bayern Munich na Manchester United .
Aubameyang alikuwa mfungaji bora wa pili kwenye ligi ya Ufaransa msimu uliopita akimaliza msimu kwa mabao 19 huku akitoa pasi 14 kwa wenzie kufunga.
Aubameyang amecheza St Ettiene kwa miaka miwili tangu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2011 toka Ac Milan ya Italia ambapo katika mechi 73 alizocheza alifunga jumla ya mabao 35.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top