Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Jo’burg, Afrika Kusini. Tangu kuanza kuumwa kwa Nelson Mandela, watu mbalimbali wamekuwa wakifuatilia mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake, mambo yote aliyoyafanya.
Wapo wengine wanaofuatilia kwa karibu hali yake kiafya, ingawa hofu imekuwa maisha nchini humo baada ya kifo chake.
Hata hivyo, miongoni mwa vivutio vikubwa ni Daraja la Nelson Mandela jijini Johannesburg.
Hili ni daraja kubwa ambalo lilikamilika kujengwa mwaka 2003, lakini kwa sasa limegeuka kivutio kwa maelfu ya wageni na wenyeji wanaolitembelea, kupiga picha za ukumbusho.
Likiwa na urefu wa mita 248, daraja hilo linapamba anga la Johannesburg kwa rangi za upinde wa mvua hasa nyakati za usiku.
Kwa ufupi, daraja hilo linatumika juu ya njia ya reli inayounganisha vitongoji vya  Newtown na Braamfontein, jirani na eneo maarufu la kibiashara lililogharimu Rand 38-milioni.
Wabunifu wake walitaka kuongeza kitu katika uzuri wa jiji hilo la kisasa, kupendezesha eneo la katikati ya jiji hili kwa kulipa sura ya kuvutia.
Lengo lake likiwa ni kuunganisha kitongoji kinachokua cha Newtown na eneo la kibiashara la Braamfontein, pia kuwezesha kuyafikia maeneo hayo kwa urahisi wakati wote.
Ujenzi wake mwanzoni ulionekana kuwa changamoto kubwa kwa timu ya wabunifu na wahandisi wake kupita eneo ambako njia 42 za reli zinapishana bila kuingilia usafiri au kusababisha misongamano ya magari.
Kwa jumla, daraja hilo la  Mandela ambalo ni ubunifu wa Kampuni ya Dissing & Weitling, ndilo kubwa la waya Kusini mwa Afrika.
Liliandaliwa maalumu kuwa jepesi, likichanganya vyuma na vifaa vingine vya kuliwezesha kuwa jepesi kwa kadri inavyowezekana, lakini lenye nguvu ya kutosha.
Kulingana na mtandao wa Engineering News,  kiasi cha mita za mraba 4,000 za zege, tani 1,000 za vyuma zilitumika kwenye ujenzi wake na tani 500  zaidi ya vyuma maalumu vya kushikilia msingi wake.
Daraja hilo si heshima pekee kwa Afrika Kusini na kiongozi wake wa kwanza wa kuchaguliwa, Nelson Mandela, bali ujenzi na muundo wake ni utambulisho wa jinsi kiongozi huyo alivyobaki kiunganishi cha raia waliotengwa na ubaguzi wa rangi.
Wengi wanalitumia daraja hilo kama njia ya kuliona vyema anga la jiji hili.  Kwa madereva wengi, wanaendesha magari juu yake au hupenda kulitazama wakiendesha kwa mwendo taratibu, kutembea juu kupitia njia ya waendao kwa miguu. Pia, kuna njia ya waendesha baiskeli ili kuhakikisha kwamba wako salama wakati wanapovuka eneo hilo la jiji lenye shughuli nyingi.
Daraja hilo lina njia rahisi ya kuliona jiji bila malipo, ingawa wageni wanashauriwa kufurahia mandhari yake kwa mguu hasa wakati wa shughuli nyingi jijini humo.
                                            mtanzania

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top