Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

1005109_484655468275725_751916481_n
Haya watu wangu wa  nguvu ni wiki nyingine tena lazima mambo yaende kama yanavyotakiwa kwenda japokuwa ni wazi kwamba Jumatatu ni siku ngumu sana kuanza kazi kwa watu wengi. Chukua muda wako kusoma hii collection ya vichekesho ili upate start up mtu wangu na kazi iende kama ulivyopanga.Mwambie na mwenzako ukimuona hapo job au chuo kama hana mood ya kazi au masomo apitie hapa apate start up kidogo.

Mume: Hello baby!
Mke: Hello swt!
Mume: Nitachelewa kurudi leo
Mke: Nishajua uko kwa vijanamke vyako, wewe ni mzinzi sana sijui ilikuaje ukanioa nakuchukia kama nini? sikupend! sikupend!
Mume: Niko BENKI hapa
Mke: Haa! Ulijuaje kama sina hela, nitolee laki 1 baby, nakupenda sana kuliko roho yangu, nakutengea maji yakuoga sweety. Usisahau hizo pesa ninunulie na chips kuku mmwaaaa! 


Mume: Ni BENKI YA KUCHANGIA DAMU
Mke: Nyoooo waambie wakutoe yote


…………………..

Mzee mmoja alichoshwa na habari za mtaani kwamba mwanaye hata umuulize swali jepesi kupita yote ni lazima atakosa !!!. Siku moja akaamua kuandaa swali jepesi kupita kiasi ili amuulize mwanae mbele ya watu kufuta ile historia mbaya. Siku ya siku ikafika mbele ya umati mshua akamuita mwanae kisha akamuuliza swali lifuatalo….. Mwanangu mtu mwenye umri wa miaka kati ya 18 hadi 35 huitwa KIJANA….. Je mtu mwenye umri kuanzia 36 hadi 50 ataitwa nani !….. Toto bila hata ya kufikili kwa sauti likajibu “ANAITWA KIJUZI”. Vp angekuwa mwanao ungemfanyaje !.

………………… 

Jamaa mmoja alienda kuomba kazi kwenye ZOO. Akaambiwa nafasi ya kazi ipo ila hakuna sokwe, hivyo utajifanya sokwe na tutakupa ngozi ya sokwe utavaa” .Jamaa siku ya kwanza akavaa, walipokuja watalii mambo yalienda vizuri. Siku iliyofuata banda lake liliwekwa kwa juu ya banda la Simba. Jamaa katika kuongeza mbwembwe akawa anarukaruka, kwa bahati mbaya si akaangukia ndani ya banda la Simba. Uwoga ukamshika akawa anapiga kelele “mama nakufaa, mama nakufaa, mama nakufaa!”. Mara yule Simba akamwambia “acha ujinga wewe kelele za nini sasa, mimi mwenyewe binadam!, rudi kwenye banda lako kabla watalii hawajaja watatushtukia.”

……………….. 

Jamaa alionekana kapona hivyo atolewe kwenye hospitali ya machizi arudishwe kwao. Asubuhi mmoja akachukuliwa na ambulance mpaka jirani na kwake, akaulizwa unapafahamu hapa? Akajibu ‘ Ndio nyumba yangu ileee”. Ghafla mlango wa nyumba ile ukafunguka wakatoka watoto wawili wamevaa yunifom,’Hee na watoto wangu walee wanaenda shule’. Mara akatoka mwanamke, jamaa akafurahi,’ Mke wangu yule, mke wangu jamani’. Madaktari walianza kumfungulia atoke kwenye gari ghafla mwanaume akatoka kwenye ile nyumba, jamaa akaangalia kwa makini kisha akaruka kwa furaha,’ Mimi yulee naenda kazini, unaona nilivyopendeza na suti ile nilinunua Mariedo’. haraka sana akarudishwa hospitalini.

……………….

Mama mdaku alishangaa kila siku mchungaji wa kanisa anaingia nyumba ya jirani yake ambaye hana mume.Akawa anajiuliza anakwenda kufanya nini? .Basi na tabia yake ya umbea uzalendo ukamshinda. Ikabidi aende kwa jirani yake na akamuuliza, ”Mwenzangu mbona kila siku mchungaji anakuja kwako? Vipi anakuja kukuombea nini?”

AKAJIBIWA:Mama huo ni umbea tuu!! Mbona kwako kila siku anakuja mwanajeshi, kwako kuna vita.?

……………..

KIBAKA alimpiga roba bubu, bubu akawa anajitetea kwa kupiga kelele:
Bubu: Abaabaabaabaa.
Kibaka, ili asijulikane kama anamkaba alimalizia naye kwa sauti ili ionekane wanaimba wimbo.
Kibaka: Prakata tumba…tumba.


……………..

ASKARI wa jiji alimkamata raia akijisadia haja ndogo hadharani tena mahali palipoandikwa USIKOJOE HAPA, FAINI SH. 5000. Raia huyo bila ubishi akatoa noti ya shilingi elfu 10 na kusubiri chenji. Askari alizunguka na kukosa chenji, akamrudia raia huyo na kumwambia:
Askari: Hebu kojoa mara ya pili umalizie fedha yako, nimekosa chenji.


……………

Uchoyo noma.

Mama mmoja alipakua chakula mara ghafla akasikia mtu anapiga hodi, ikabidi afiche chakula chini ya kochi.
Mgeni alipoingia ndani na kukaa kidogo akaona moshi unafuka chini ya kochi, akauliza “Moshi wa nini huo?”
Mama mchoyo akajibu haraka haraka ” Mwenzangu utaiweza mipanya ya humu ndani  kwa bangi na sigara inavuta kama binadamu.”


……………….

Teja alimtokea Binti mzungu akamwambia,
“I love you”
Mzungu akajibu,
“I love you too”


Jamaa akamwambia,
“I love you three”
Mzungu akaduwaa akamuuliza,
“What for?”


Jamaa akasema,
“What five”
Mzungu akashangaa akamuuliza,
“Are you sick?


Teja akamjibu
“Are you seven?
Mzungu akamwangalia kisha akamwambia,
“I hate you”


Teja hataki kushindwa akasema,
“I nine you”.


………………

WAZO LA JUMATATU

kumbuka hata nyumba ina paa ila haitui airport

Hata uwe na haraka kiasi ganI, huwezi kuomba lifti kwenye gari la takataka

Hata uwe msafi vipi, huwezi kunawa mikono wakati wa kula rushwa

Kaa ukijua hakuna baba mwenye gari ila kuna baba mwenye nyumba

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top