Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakare akionyesha alama vidole katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
HATIMAYE Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilfred Muganyizi Lwakatare aamepata dhamana na kurudi uraiani, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuamua kuwa dhamana yake iko wazi.
Mwandishi wa Habarimpya.com akiwa katika viwanja vya Hahakama hiyo anasema kwamba, Lwakatare amepata dhama hiyo yenye dhamani ya tsh 10milioni pamoja na kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika na kukabidhi hati za kusafiria Mahakamani hapo.

Awali Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka manne, matatu kati yake yakiwa ya ugaidi na moja la kawaida la jinai, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakidaiwa kula njama na kupanga kumteka Dennis Msacky na kisha kumdhuru kwa kutumia sumu. 
Hata hivyo, Mei 8, mwaka huu Jaji Lawrence Kaduri wa Mahakama Kuu aliwafutia mashtaka hayo matatu ya ugaidi na kuwabakizia shtaka moja linaloangukia kwenye jinai ya kula njama za kutenda kosa la kumdhuru Msacky kwa kutumia sumu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top