Miss Tanzania mwaka 2006 na muigizaji
wa filamu Wema Sepetu amefunguka kupitia jarida jipya la Mzuka kuwa
katika uhusiano wake wote na Diamond hakuwahi kumsaliti.
Wema ambaye yupo kwenye cover la
jarida hilo linalotolewa na Bongo5,amefunguka kwa kusema kuwa yeye na
Diamond walikuwa wakipendana sana.
“Maisha yangu yote tangia nimeanza
mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to
be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb
nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo,” amefunguka Wema.
Wema amefunguka pia kuhusu jinsi
Diamond alivyomcheat na Jokate kwa kusema, “nadhani pia inacost mwanaume
akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani
au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya
Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza.”
Katika jarida hilo ambalo linauzwa
kwa shilingi 1,500 tu, Wema amesimulia mengi tangia alipokutana na
Diamond, jinsi alivyoumizwa na kitendo chake cha kumrekodi na kusambaza
sauti kwenye radio, mapenzi yake na Kanumba, utajiri wake, jinsi
anavyowapenda mbwa wake na mambo mengine exclusive.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment