
Inawezekana umeshakutana na wasichana
warembo sana zaidi ya hawa, lakini leo hebu tuwatazame hawa watatu
wanaowakilisha nchi tatu za Africa Mashariki yaani Kenya, Tanzania na
Uganda. Leo hatuangalii nani ana pesa ngapi katika bank account yake,
wala anamiliki nini, tunaangalia kitu kimoja tu, yupi ni hot zaidi ya
wenzake??
Hawa ni kati ya wasichana warembo na
maarufu East Africa (bila ubishi) hususan kila mmoja katika nchi
anakotoka kutokana na kuwa kwenye spotlight.
Tukianza na Vera Sidika anafahamika
pia kama Vee S Beiby, ni mwanafunzi, model, na mjasiriamali. Vera
ameshawahi kushiriki katika video za wanamuziki wakubwa Kenya akiwemo
Prezzo na kundi la P-Unit kupitia wimbo wao wa ‘You Guy’ alitokea kama
video model.
Kutoka Tanzania ni Agnes Gerald
ambaye amepata a.k.a ya Agnes Masogange kutokana na kushiriki katika
video ya wimbo ‘Masogange’ ya msanii wa R&B Belle 9 ambayo
ilimuongezea umaarufu mara dufu, ameshatokea pia katika video nyingine
kadhaa hapa Tanzania. Agnes ni model.
Kutoka Uganda here is the sexy boss
lady Zari Hussein, huyu ni mwanamke mrembo ambaye baba yake ni
mchanganyiko wa Burundi na Somalia, na mama yake ni mchanganyiko wa
India na Mutaaro. Zari ni ufupisho wa jina lake kamili Zarinah Zaitun
Hussein. Mrembo huyu ni mwanamuziki japo hajapata mafanikio makubwa sana
kupitia muziki.
hebu chukua sekunde zako kadhaa
kutathmini kila idara ya uzuri wa warembo hawa watatu kisha tupia
comment yako chini tuambie nani unadhani ni ‘hot’ kuliko wenzake?
Credits: Zedylicious blog
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro



















Post a Comment
Post a Comment