Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Silvio Berlusconi, former prime minister of Italy, reigning world champion skeezebag. Waziri mkuu wa zamani wa Italia ambaye pia ni mmiliki wa klabu ya Ac Milan Silvio Berlusconi amehukumiwa kifungo cha miaka 7 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha kwenye ngono na mabinti walio chini ya umri wa miaka
18.http://t3.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcRZWg7ciFwTR_QAxqzTS5169wlsjFfxoQzHQMS3YLDjPYetCtO-
Zaidi ya hapo Berlusconi ambaye amewahi kuiongoza Italia kama waziri mkuu kwa vipindi vitatu tofauti amefungiwa kutojihusisha na siasa kwa maisha yake yote kufuatia kashfa hiyo .
http://blogs-images.forbes.com/luisakroll/files/2012/10/Silvio-Berlusconi.jpg
Hukumu hii ni ya tatu kwa Silvio ndani ya kipindi cha miezi tisa iliyopita ambapo mwezi oktoba mwaka 2012 alihukumiwa miaka minne gerezani kwa kukutwa na hatia ya ukwepaji wa kodi na miezi miwili baada ya hapo alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kutumia ushahidi wa kunasa mazungumzo ya simu kinyume cha sheria .
Berlusconi anatarajiwa kukata rufaa juu ya hukumu ambayo hata hivyo haina nafasi kubwa ya kufanikiwa kutokana na kashfa zinazomzunguka ambazo zinafanya iwe vigumu kwake kusafishika .NA MILLAD TZA

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top