
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema
Serikali imetambua umuhimu wa Watanzania kuruhusiwa kuwa na uraia wa
nchi mbili. Hatua hii imepelea Serikali kupendekeza kwenye Tume ya
Mabadiliko ya Katiba ili suala hilo lifikiriwe kuingizwa kwenye Katiba
Mpya ambayo mchakao wa kuiandaa unaendelea.
Waziri
Membe aliyasema hayo alipokuwa akiwasilisha Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara yake mwaka 2013/14 kwenye mkutano wa kumi na moja wa
Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Alisema suala la uraia wa nchi mbili limekuwa likiwatatiza Watanzania walioko nje ya nchi kwa mambo mengi, ikiwamo kujihusisha kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo nchi wanazoishi.
Waziri Membe alisema Wizara yake katika maoni yake kwa Tume ya Katiba, ililipa suala la uraia wan chi mbili kipaumbele kwa kuamini kuwa hatua hivyo itwawezesha Watanzania waliopo nje kuchangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya nchi yetu kama inavyofanyika katika nchi zingine ambazo sheria hiyo inatumika.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment