Waziri Mkuu wa India,Manmohan Singh Reuters/Danish Siddiqui |
Na Lizzy Anneth Masinga
Takriban Watu 60 wanahofia kupoteza maisha wengine maelfu wakiachwa bila
makazi baada ya mvua kubwa kunyesha na kubomoa nyumba na kuharibu
barabara kaskazini mwa India.
Shughuli za uokoaji zimeanza Mamlaka ikitumia Helkopta za kijeshi
kujaribu kuaokoa wakazi walionasa kutokana na Mafuriko na maporomoko ya
udongo yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha kwa zaidi ya siku tatu
katika jimbo la Uttarakhand.
Waziri anayeshughulika na majanga na uokoaji amesema kuwa wameshindwa
kuthibitisha idadi ya Watu waliopoteza maisha kwa kuwa miundo mbinu ya
Mawasiliano imeharibika .
Picha za Televisheni zimeonesha Madaraja na nyumba zikianguka kisha kuzolewa na maji yenye kasi.
Miundombinu ya Barabara imeharibiwa, huku ikiwaacha mamia ya waumini
waliokuwa wakielekea kwenye nyumba ya kuabudu wakiwa katika hali ya
sintofahamu.
Katika maeneo mengine mvua zilizokuwa zimeendelea kunyesha zimesababisha
zoezi la uokoaji kuwa gumu , huku Waokoaji kutoka kitengo cha taifa cha
kupambana na Majanga nchini India wakisubiri kutekeleza jukumu hilo kwa
njia ya anga.
Mvua za masika nchini India, hutegemewa sana na Sekta ya Kilimo nchini
humo mvua ambazo hunyesha kuanzia mwezi June mpaka mwezi Septemba
zikisababisha mafuriko.
Via kiswahili.rfi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment