Arusha kimenuka: polisi waamua kutumia mabomu ya machozi na kupiga raia
Polisi wanapiga mabomu ya machozi. Kuna gari limepigwa bomu mpaka limefumuka
============================== =====
UPDATES KUTOKA KWA MEMBERS WENGINE
============================== =====
By
Arushaone
Polisi wameanza kupiga mabomu wakati wabunge wa
CHADEMA walipoanza kuhutubia maelfu kwa maelfu ya wafuasi wake. Hali ni
mbaya sana hata watu wametelekeza magari na pikipiki zao, wabunge wote
nao wamekimbia na mbaya zaidi wanapiga mabomu kila mahali.
By
kakuku
Hali ni tete, mabomu yanarindima sana hali ni
tete magari ya mevunjwa gari la Lissu laharibiwa, pikipiki zinavunjwa na
polisi bila sababu. Hali tete, tegemeeni msiba mwingine
By
Arushaone
Wametumia risasi za moto kupiga watu, gari la
Tundu Lissu limevunjwa vioo na jeshi la polisi. Wameumiza watu wengi
sana! Hali ni mbaya sana!
By
Gsana
Kufuatana na mgogoro wa serikali na wananchi wa
Arusha, barabara inayounganisha kalolen na polisi central mpaka pale
benki kuu arusha pamefungwa na inaonekana kuna pilikapilika nyingi
central zinazoashiria hali si shwari Huku upande walipo wanaCHADEMA
kukirindima mabomu...
Tahadhari wanaJF, msipite barabara hiyo kuanzia muda huu saa kumi na nusu ya tar 18 June 2013.
By
Ciril
Kwa kweli hali ni ya hatari na wabunge kadhaa
wa Chadema wameshikiliwa, polisi wanatumia nguvu kubwa kupita kiasi.
Baadhi ya vyombo vya usafiri vilivyoachwa eneo la tukio polisi
wanaviharibu kadiri wawezavyo. Usafiri wa abiria katika barabara ya
Moshi-Arusha umesitishwa na hakuna gari zinazopita latika barabara hiyo.
Majeruhi ni wengi na wamepelekwa hospitali.
Mabomu yalilipuliwa baada ya naibu mwenyekiti kuhitimisha kwa kuwaomba
wananchi waliojikusanya eneo la Soweto waende ktk hospitali ya Mount
Meru kwa ajili ya kwenda kuwaaga marehemu. Awali palitokea mabishano
kati ya polisi na viongozi wa Chadema kuhusu mkusanyiko uliokuwapo hapo.
Polisi walisema AICC wamekataa uwanja wao wa Soweto usitumike ktk
shughuli yoyote. Bado vyombo vilivyoachwa uwanjani na wananchi
vinaendelea kuharibiwa na polisi na baadhi ya wananchi wamejificha ktk
fensi na baadhi ya nyumba zilizopo ktk uwanja huu.
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment