Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Nchini (Tacaids) imesema tafiti
mbalimbali zinaonyesha kuwa vitendo vya ngono kinyume na maumbile
vinazidi kuongezeka.
Hayo yalisemwa jana na Dk. William Kafura, katika mkutano wa sita wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Ukimwi (Tapac).
Alisema hiyo inatokana na imani za kishirikina kwamba wakifanya vitendo hivyo watapata bahati kwa kupandishwa vyeo.
“Lazima tukubali tatizo lipo na
tulitafutie suluhisho, utafiti upo umefanywa na Muhimbili, umefanywa na
chuo kikuu cha Dar es Salaam, umefanywa na Tasisi ya Utafiti ya
Ifakara,”alisema.
Alisema pia wafanyabiashara wanaamini kwa kufanya vitendo hivyo watajirika wakati wanawake wanaamini kuwa watazidi kupendwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TACAIDS, Dk. Fatuma Mrisho, alisema
utafiti uliofanyika nchini unabainisha kuwa wanawake hawana uelewa wa
kutosha juu ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi.
Akizungumzia suala la kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi Dk. Mrisho alisema
kuwa wanaume wana uelewa mkubwa zaidi kuhusu ugonjwa huo kuliko
wanawake.Hata
hivyo, alisema kwa sasa ipo kazi kubwa ya kutoa elimu kwa wananchi na
hivyo kuwataka wabunge na viongozi mbalimbali kutoa elimu juu ya
kujikinga na gonjwa hatari la ukimwi.
Aidha Mrisho alisema kuwa kwa sasa Mkoa wa Njombe unaongoza kwa
maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwa asilimia 14.8 ambapo Unguja
Kaskazini inamaambukizi madogo kwa asilimia 0.1.
Hata hivyo alisema kuwa kuna changamoto mbalimbali ambazo wanakumbana
nazo ni pamoja na rasilimali za ukimwi kwa serikali, mashirika ya Dini
na sekta binafsi kuwa pungufu kuliko mahitaji.
Alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto lakini nia ni kufikia sifuri
tatu ifikapo mwaka 2015 na hiyo hipo katika ulimwenguni, Afrika hapa
hapa Tanzania.
CHANZO:NIPASHE
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment