MTANGAZAJI
wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amewashangaza
watu baada ya kutundika mtandaoni picha zinazomuonesha akioga bafuni
huku nyingine akiwa chooni akikata gogo.
Picha
hizo zinapatikana kwenye mtandao wake na hakueleza ilikuwa wapi ila
akasema ilikuwa ni siku alipoamua kuitumia wikiendi yake ipasavyo katika
hoteli ambayo hakuitaja jina.
Baadhi
ya watu waliyoziona picha hizo walimponda wakidai eti ni ulimbukeni
lakini wapo waliomtetea kwa kusema, ni staili tu ya maisha aliyoamua
kuishi.
“Ushamba
tu, ndo nini sasa? alisema mmoja wa wadau huku mwingine
aliyejitambulisha kwa jina la Dick akisema: “Msimuonee wivu mwenzenu,
anakula bata zake na nyie hamjakatazwa.”
Dida
alipoulizwa kuhusu kujianika hivyo alisema, hizo ni ishu zake binafsi
na wapenzi wake wanapenda kuona kila anachokifanya, ndiyo maana
anawawekea kwenye blogu yake
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro










Post a Comment
Post a Comment