Mbunge wa
Kawe (Chandema), Halima Mdee ameanza maandalizi yake ya pambano la ngumi dhidi
ya staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper.
Pambano la
wakali hao litafanyika Julai 7, siku ya Sabasaba katika Tamasha la Matumaini
kwenye Uwanja we Taifa jijini Dar es Salaam.
Mdee
amekuwa akiendelea na mazoezi yak echini ya Mbunge wa CCM, Idd Azzan ambaye pia
siku hiyo atapanda ulingoni kutoana jasho na mkali wa Bongo Movie Jacob Steven ‘JB’
Katika tamasha
hilo mwaka jana Wolper alionyesha uwezo kuliko Wema Sepetu katika pambano lao
lililosisimua.
Lakini Mdee
ametamba kumpoteza Wolper katika pambano lao hilo la Julai 7.
Mdee
anaendelea na mazoezi mjini Dodoma, wakati Wolper anaendelea na mazoezi jijini
Dar es Salaam.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment