Wakali wa bongo
fleva wenye vocal zenye ladha na nguvu ya aina yake Lady JayDee
‘Anaconda’ na Q-Chillah, wamekutana tena studio kurekodi wimbo mpya
ikiwa ni miaka kadhaa imepita walipotisha na wimbo wao ‘Zamani’.
Lady
JayDee alipost picha kupitia akaunti yake ya Twitter ikimuonesha yeye na
Q-chilla wakiwa ndani ya studio za Combination sound na Man Walter, na
kuisindikiza na maelezo.
"Mtu 3 ndani ya
studio. Mwaikumbuka Zamani - Q Chief feat Jide?? Nikilala naotaa, naota
km unaniita. Sasa yaja mpya."Alitweet Jide June 26.
Hakuchelewa
kutaja jina la wimbo huo “Sukari” na kuonesha kuikubali sana, hii inatoa
picha kuwa kitu kikubwa kinakuja.
“Sukari - Qchillah & Jide another hit ???
☺ #Justasking.” Aliongeza.
Tuisubiri hiyo sukari tuonje ladha yake kwa masikio.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment