KIUNGO wa Simba ambaye anatakiwa na klabu ya Raja Casablanca ya
Morocco, Amri Kiemba amewaambia viongozi wa klabu hiyo kwamba
hajafurahishwa kuachwa kwa kipa namba moja, Juma Kaseja.
Kiemba ambaye amesaini mkataba na Simba kwa Sh.35
milioni, amesisitiza kuwa uamuzi uliofanywa dhidi ya Kaseja kwa mtazamo
wake si sahihi labda kama kuna sababu nyingine ya nje ya uwanja.
“Sijafurahishwa na uamuzi waliofanya viongozi wa
kumuacha Kaseja, kusema kweli si sahihi kwa sababu Kaseja bado naamini
ni kipa mzuri na ana uwezo mkubwa sana na isitoshe hakuna sababu ya
maana iliyowafanya wamuache labda kama kuna sababu nyingine pembeni na
si ya kisoka,” alisema Kiemba ambaye aliwahi kucheza Yanga.
Aliongeza: “Hili jambo nimelisikia tu juu juu
ingawa sasa naanza kuamini ingawa viongozi kokote walipo wajue
hawajatenda haki bado alistahili kuichezea timu hii.”
Kaseja alianza kuichezea Simba mwaka 2003 akitokea
Moro United na aling’ara mwaka huo wakati wa Ligi ya Mabingwa Afrika na
kuiingiza klabu hiyo kwenye raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya
kuitoa Zamalek ya Misri kwa penalti.
Simba wamethibitisha kupitia kwa Mwenyekiti wa
klabu, Ismail Aden Rage na bosi wa usajili, Zakaria Hanspope kwamba
hawatampa Kaseja mkataba mpya na kwamba akatafute timu nyingine.
mwanaspoti.
mwanaspoti.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment