Nyota wa tasnia ya filamu , Jaqueline
Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai kuwa hawapendi sana wanaume wenye fedha
kwani wengi wao ni waume za watu...
Wolper anadai kuwa nao si rahisi kuonyeshwa mapenzi yao ya dhati kwani mapenzi yao ni ya chumbani tu...
" Unajua unapokuwa na mtu mwenye
fedha zake , alafu mtu mzima, ni lazmia ukose penzi la kweli kwani
mapenzi yenu ni chumbani tu, hamuwezi kutembea pamoja kukaa kama vile ni
wapenzi ...
"Lakini ukiwa na kijana ambaye hana
pesa na wewe una kazi lazima akuonyeshe jinsi mapenzi yalivyo kwa
kukuweka karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake..
“Wanaume wengi wenye pesa zao huniona nina dharau, lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke .
"Kuna watu wanaamini pesa zao ndio
kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo , ukileta mapenzi hayo lazima
unione nina dharau”,anasema Wolper Gambe.
Wolper anadai kuwa kuna watu ambao
huwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni
Malaya lakini wanasahau kama nao ni binadamu na wanaroho kama wanadamu
wengine....
Jack Wolper anasema wao si malaika ,
wanapenda na kupendwa, kwa hiyo ukimuona ana kijana Serengeti boy ujue
ni kwa ajili ya kupata penzi nzito na kusikilizwa haja zake.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment