Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kajala Mwigizaji aliyerudi uraiani hivi karibuni Kajala Masanja amefanya mabadiliko makubwa ya mtindo wake wa nywele baada ya kunyoa kipara “kikavu” kichwani mwake. Katika picha alizozitoa mwigizaji huyo kupitia kwenye mtandao leo jioni, mwigizaji huyo ameonekana akiwa na kipara tofauti na alivyozoeleka na nywele nyingi siku za nyuma.
Bongomovies.com tuliamua kumtafuta mwanadada huyu ili kujua “kunani”?? na staili hiyo na tulimpigia simu na maongezi yalikuwa kama ifuatavyo:
Bongomovies.com: Mambo kajala, mzima?

Kajala: Mzima, kwema?
Bongomovies.com: Kwema kabisa, vipi tena na kipara kichwani?
Kajala: Aha,..Siunajua tena mishe mishe, nipo na shoot movie yangu mpya ndo mana imenibidi ninyo kipara maana inanilazimu kuonekana hivyo ndani na Filamu hiyo.
Bongomovies.com: Okay, na itaitwaje?
Kajala: Itaitwa Heart attack
Bongomovies.com: Umewashirikisha nani na nani humo ndani?
Kajala: Atakuwepo Hemedi na mastaa wengine Kibao, kifupi ni bonge la movie yani.
Bongomovies.com: Basi tunaisubiri kwa hamu sana
Kajala: Pamoja sana.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top