Walipuaji mabomu wa kujitoa muhanga na watu wenye silaha wa al-Shabaab
walishambulia eneo la Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu siku ya Jumatano
(tarehe 19 Juni), na kusababaisha vifo vya angalau watu wanane.

Askari na wahudumu wa dharura wakitafuta
ndani ya kifusi nje ya ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu muda
mdogo baada ya al-Shabaab kulishambulia siku ya Jumatano (tarehe 19
Juni). [Na Dahir Jabril/Sabahi]
Kwa uchache raia watatu waliuawa katika mitaa nje ya majengo hayo wakati
majeshi ya Somalia na Umoja wa Afrika yalipojaribu kuingia ndani katika
majengo hayo ili kumaliza kuzingirwa kwa saa moja na nusu, AFP
iliripoti na kuongezea kwamba wakandarasi watatu wa kigeni na kiasi cha
walinzi wa usalama wawili wa Somalia waliuawa wakati wa shambulio hilo.
Shambulio hilo lilianza mnamo saa 10:30 asubuhi saa za eneo hilo wakati
gari la al-Shabaab lililokuwa limejaa milipuko lilipolipuliwa nje ya
milango ya eneo la UN katka wilaya ya Hodan ya Mogadishu, kwa mujibu wa
wafanyakazi wenyeji wa UN waliozungumza na Sabahi.

Gari iliyokuwa ikipita katika maeneo ya UN
ilijigonga karibu na makazi ya karibu wakati mlipuko hupo ulipotokea.
[Na Dahir Jibril/Sabahi]
Wapiganaji sita wa al-Shabaab waliingia katika eneo hilo na kuanza
kufyatua risasi na kutupa mabomu ya mkono kwa maafisa wa ulinzi katika
uwanja wa ndani. Askari wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia
(AMISOM) walifika katika eneo la tukio chini ya dakika 15, na mapigano
makali yalizuka baina yao na wanamgambo kwa zaidi ya saa moja.
Washambuliaji hao, hata hivyo, walishindwa kuingia ndani ya ofisi yoyote
na kujilipua wenyewe walipoishiwa na risasi, mashuhuda waliiambia
Sabahi, na kuongeza kwamba mmoja wa wanamgambo wa al-Shabaab alikamatwa
akiwa hai.
Sadiyo Muse, mwenye umri wa miaka 32 na mkaazi katika kitongoji cha
Taleh cha Hodan, alisema kuwa dakika chache kabla ya mlipuko kutokea
alikuwa amezungumza na baba yake ambaye alikuwa anatembea mbele ya
majengo hayo akiwa njiani kwenda kutembelea jamaa wanaoishi karibu.
Muda mchache baada ya mlipuko, jamaa yake alimweleza kuwa majengo ya UN yameshambuliwa na hivyo akakimbilia eneo la tukio.
"Niliutambua mwili wa baba yangu uliokuwa umeungua mbele ya lango kwa nguo zake," aliiambia Sabahi.
"Nimeshtushwa sana na kutishwa na kile kilichotokea mjini Mogadishu
leo," alisema Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa UN kwa Somalia
Nicholas Kay. "Eneo la Pamoja la UN lina wafanyakazi wanaofanya kazi
katika masuala ya ubinadamu na maendeleo kwa watu wa Somalia. Hili
lilikuwa tendo la kigaidi na jaribio la kukata tamaa la kuigonga Somalia
nje ya njia yake ya kurejea kwa hali na ujenzi wa amani."
Mamia ya wafanyakazi wa UN wanafanya kazi katika majengo haya, iliyo na
ofisi kadhaa ya mashirika ya UN yakiwemo ya Shirika la Chakula na
Kilimo, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, kamishna Mkuu wa UN wa
Wakimbizi, na Afisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu.
Mashirika mengine ya UN, ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Kuokoa Watoto,
ambao pia una ofisi zake hapa, za majengo kumi ya gorofa tatu. Wakati wa
mapigano ya wazi, waajiriwa walikuwa wamejifungia chini na walikaa
mbali na madirisha.
Al-Shabaab ilidai kuhusika na shambulio hilo kupitia Twitter.
"Kitengo cha Mujahidina kutoka Brigedi ya Ushahidi kimevamia eneo la
UNDP karibu na uwanja wa ndege mjiini Mogadishu," ilisema siku ya
Jumatano.
"Umoja wa Mataifa, mfanyabiashara wa kifo na nguvu ya shertani mwovu,
mwenye rekodi nyingi za fedheha za kutoeneza chochote zaidi ya umaskini,
utegemezi na ukafiri," al-Shabaab walisema katika jaribio la
kuhalalisha umwagaji damu na upotevu wa maisha.
"Mashambulio haya yasiyo na mafanikio ya al-Shabaab yanadhamiria tu
kwenye kuvuruga jitihada zinazoendelea za watu wa Somalia kujiondoa
katika miaka ya vurugu nchini Somalia na hautazuia kwa kutia hofu
jitihada za pamoja kuendelea kusaidia watu wa Somalia kujenga tena nchi
yao," alisema Mwakilishi Maalumu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa
Afrika kwa balozi wa Somalia Mahamat Saleh Annadif.
Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon pia amelaani shambulio hilo muda mchache baadaye.
"Ninalaani shambulio lisilo na maana na baya kwa raia wasio na hatia wa
Umoja wa Mataifa asubuhi hii," alisema katika kauli yake. "Umoja wa
Mataifa ni rafiki na washirika wetu, na mashirika ya Umoja wa Mataifa
yanatupea msaada wa kibinadamu na usaidizi, hivyo, mimi na Wasomali wote
tumeshtushwa kwamba wamekuwa walengwa na waathirika wa vurugu hizo za
kikatili."
Ofisi ya waziri mkuu na Umoja wa Mataifa hazikuweza kuthibitisha idadi ya waliouwawa au majeruhi siku ya Jumatano.
"Kwa huzuni tunapaswa kusubiri kusikia maelezo kamili na uthibitisho wa
waliouwawa au majeruhi yeyote," alisema Shirdon. "Mawazo yetu yote na
sala ni pamoja na wenzetu wa UN leo. Lakini al-Shabaab hawataiangusha
mchakato wa amani. Hawatasimamisha ahueni wetu. Vurugu hazitashinda."
Shambulio kubwa la mwisho la al-Shabaab huko Mogadishu lilikuwa mwezi
Aprili, wakati kikosi cha makomando wa kujitoa mhanga walipojilipua
wakiwa njiani kuelekea kwenye jengo la mahakama kuu ya Mogadishu, na
kusababisha vifo vya watu 29.
"Wasomali wanawakataa al-Shabaab. Wakati sisi na UNSOM tunaijenga upya
Somalia, hawaleti chochote zaidi ya maumivu na uharibifu. Mungu
atawalaani," Shirdon alisema katika mtandao wa Twitter.
Chanzo: sabahionline.com
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment