
Jupp Heynckes anaweza kurudi Real Madrid msimu ujao, Agent wa kocha huyo amethibitisha suala hilo jana.
Heynckes amefanikiwa kutwaa kombe la Ulaya kwenye uwanja wa Wembley jumamosi na atashiriki kwenye mechi ya mwisho mwisho wa juma hili na timu ya Stuttgart kwenye kombe la Ujerumani kabla ya kurithiwa na Pep Guardiola.
Baada ya kocha wa sasa wa Madrid amethibitisha ataondoka Bernabeu mwisho wa msimu, Heynckes anahusishwa na kwenda Spain japo kocha wa sasa wa timu ya PSG Carlo Ancelotti anapigiwa chapuo kuchukua kazi.
Mchezaji huyo wa zamani wa Ujerumani Magharibi amewahi kuifundisha timu hiyo ya Real Madrid mwaka 1997 na kutwaa kombe la Ulaya na kombe la mfalme.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment