Kocha wa Manchester United anayestaafu Alex Ferguson Mei 12, 2013.
Sir
Alex Ferguson aliyetangaza kustaafu mwishoni mwa msimu huu ataingia
katika mabuku ya kumbukumbu kwa kujizolea sifa kochochoko katika taaluma
yake ya ukufunzi kwa kipindi cha miaka 26 akinoa Manchester United.
SIR Alexander Chapman Ferguson
'Fergie’ aliyetangaza kustaafu mwishoni mwa msimu huu ataingia katika
mabuku ya kumbukumbu kwa kujizolea sifa kochochoko katika taaluma yake
ya ukufunzi kwa kipindi cha miaka 26, akiinoa klabu moja; Manchester
United!
Sio sifa tu bali pia fedha alizojikusanyia kwa kipindi hicho zilimweka miongoni mwa makocha matajiri duniani.MAISHA YAKE BINAFSIFerguson
aliyezaliwa Desemba 31, 1941 alimwoa mkewe Lady Cathy Holding
1966.Wawili hao walijaliwa watoto watatu Mark 45, Darren na Jason 41
ambao ni mapacha.
Darren
aliwahi kuchezea kikosi cha Manchester United miaka ya tisini kabla ya
kufuata nyayo za babake za ukufunzi. Kwa sasa anainoa klabu ya
Peterborough United.
FEDHA
Kwa mujibu wa
orodha ya Sunday Times Sport Rich List 2013, Fergie ndiye kocha tajiri
nchini Uingereza akikadiriwa kuwa na utajiri wa Sh4.4 bilioni huku
akipokea ujira wa Sh858 milioni kila mwaka.
Roy Keane mchezaji wake wa zamani, sasa akiwa mkufunzi anafuata orodha hiyo kwa Sh3.8 bilioni.
Arsene
Wenger pia yuko katika nafasi hiyo huku Roberto Mancini akitamatisha nne
bora kwa Sh2.7 bilioni. Duniani, anaorodheshwa katika nafasi ya tatu
miongoni mwa makocha wanaolipwa mshahara mkubwa, Jose Mourihno anaongoza
kwa Sh1.3 bilioni, Mancini akiwa katika nafasi ya pili kwa Sh975,
Wenger akiwa wa nne kwa Sh780 milioni naye Carlo Ancelotti akihitimisha
tano bora kwa Sh650 milioni.
Utajiri wa
Ferguson unasemakana kuwa nusu ya ule wa dereva mashuhuri wa langalanga,
Lewis Hamiliton anayeorodheshwa wa tatu miongoni mwa madereva matajiri
wa langalanga duniani akimiliki Sh7.8 bilioni.
MAJUMBA
Fergie
anamiliki jumba la kifahari lililojengwa kwa kipande cha ardhi cha ekari
1.5 jijini Macclesfeild, Uingereza. Analo jumba jingine mjini Wilmslow,
Cheshire anakoishi na mkewe Cathy.
MAGARI
Licha ya kuwa
mkwasi, kocha huyu hajaonekana kuvutiwa sana na umiliki wa magari mengi
ya kifahari kama nyota wengi wa soka. Ferguson amewahi kunukuliwa
akisema kuwa hapendi kuendesha magari sana kwa kuwa huhofia usalama
wake, huenda ikiwa ndio sababu ya yeye kutopenda magari.
Hata hivyo,
magari mawili ya kifahari yanayojulikana kuwa yake ni Audi A8
lililomgharimu Sh11 milioni na Chevrolet Volt lenye gharama ya Sh4.6
miloni. Gari hilo hutumia nguvu za umeme baada ya kutiwa chaji kwa masaa
24. Pia hutumia petroli hasa chaji inapokwisha.
UWEKEZAJI
Tajriba yake
ya miaka mingi kama meneja wa klabu kubwa inayozoa faida ya mamilioni ya
pesa kila mwaka ilimpa maarifa mengi ya uwekezaji. Utajiri wake
hautokani tu na soka bali pia na biashara anazoendesha.
Yeye ni
mwanachama na mshikadau katika kampuni za filamu za Eclipse 35, Clyde
Films, Cherwell Films na Scotts Atlantic Partners. Pia anamiliki kampuni
ya kibinafsi ya mchezo wa uendeshaji farasi, farasi wawili 'What A
Friend’ na 'Harry The Viking’. Kampuni yake hujisajili kwenye mashindano
kadha ya farasi kila mwaka.
MIGOGORO
Kutokana na
msimamo wake mkali wa kiukufunzi na presha ya kuwa meneja wa klabu ya
hadhi ya Manchester, ingekuwa vigumu kwa Fergie kutotofautiana na wengi
kwa kuwakashifu, miongoni mwao ni wachezaji, shirikisho la soka la
Uingereza, FA, makocha wenzake na hata baadhi ya marefa.
Kwa kipindi cha miaka 26, Fergie alikuwa amejihusisha na migogoro mingi, haya ni baadhi yayo atakayokumbukwa sana kwayo.
Mnamo 1997
kocha wa Arsenal, Arsene wenger alipojiunga na klabu hiyo ya Uingereza
akitokea ile ya Nagoya Grampus nchini Japan, Fergie alimtaja kama
limbukeni katika taaluma ya ukufunzi na akamtaka kila anapotoa maoni
yake kuhusu hali ya soka nchini Uingereza, aelewe kwamba soka ya
Uingereza sio sawa na ile ya Japan.
Hali hii ilizua chuki kubwa baina yao na hata kuchochewa zaidi na ushindani mkali baina ya timu zao.
Miaka 10
baadaye, uhasama huo ulififia hasa Arsenal ilipoanza kupata matokeo duni
na kupunguza ushindani. Mwaka 2004, Fergie aliapa kutozungumza kamwe na
shirika la habari la BBC baada ya chombo hicho cha habari kuangaza
kipindi kilichomkashifu mwanawe Jason ambaye ni wakala wa kandanda.
Alitaja kipindi hicho kuwa cha uvumi mtupu uliolenga kumshusha hadhi mwanawe.
Desemba mwaka
huo, kocha huyo alisema kuwa hawezi kuiuzia klabu ya Real Madrid ya
Uhispania chochote hata kama ni 'virusi’ ila kufikia Juni mwaka huo
alikubali kuuza David Beckham kwa klabu hiyo na baadaye kuwauza
wachezaji wengine mahari akiwemo Cristiano Ronaldo, Rud van Nestroy na
Gabriel Heinz.
Zaidi ya
Wenger, amezozana na wakufunzi wengine kama Sam Allaydace, Allan Pardew
(alipotaja klabu yake ya Newcastle United kama duni). Chuki yake na
Rafael Benitez wa Chelsea ilidumu kwa zaidi ya muongo mmoja.
Benitez
alipokuwa akiinoa Liverpool hadi 2010, alimkashifu Ferguson kwa kuandaa
orodha ya mambo 10 kumhusu Ferguson hasa akimtaja kama mtu mwenye
majitapo anayejiona kujua kila kitu. Fergie aliyapuuza na kumtaja
Benitez kama mpuuzi.
Mchezaji
aliyewahi tofautiana vibaya sana na kocha huyu kwenye taaluma yake ni
Beckham. Beckham alimjibiza vibaya kocha huyo kwenye chumba cha
wachezaji, naye kocha huyu akamtandika usoni na daluga.
Baadaye
Fergie alimkashifu kwenye vyombo vya habari kwa kusema kuwa mchezaji
huyo alibadili tabia baada ya kumwoa mkewe Victoria ambaye ni mwanasana.
Beckham aliuzwa baadaye kufuatia tofauti hiyo.
FA imemtoza
faini ya mamilioni ya pesa na pia kumpiga marufuku ya kuhudhuria baadhi
ya mechi, zaidi ya mara saba kwa kuwakashifu wasimamizi wa michuano
mbalimbali.
Aidha, kukashifu usimamizi wa shirikisho hilo umemtia matatani.
Pia amekuwa
na cheche za maneno kwa klabu ya Manchester City, majirani na mahasimu
wao. Baada ya klabu hiyo kufaulu kumshawishi straika Carlos Tevez
kujiunga nayo kutoka Man United, kocha huyo ambaye alitaka sana kusalia
na mchezaji huyo aliisuta klabu hiyo kwa kusema kuwa kumchukua mchezaji
huyo hakungeathiri klabu yake kwa vyovyote na City haipaswi kujigamba
sana kwani ni klabu ndogo wala haiwezi kuifikia hadhi ya United.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment