Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Katika kile kinachoonekana kama mwendelezo ama tabia za wanawake kuibiana wapenzi hasa hawa wenye majina makubwa nchini, mwigizaji wa bongo movies Salma Jabu al maarufu kama Nisha, naye amegoma kumtaja mpenzi wake hadharani kwa madai ya kuwa anaogopa kunyang'anywa tena mpenzi wake huyo kama ilivyotokea alipokuwa na mpenzi wake wa zamani "Nay wa Mitego''-msanii maarufu wa bongo fleva nchini amabye naye kipindi cha nyuma likuwa mwigizaji.

 
Akiongea na gazeti moja maarufu la udaku nchini, Nisha amesema kuwa amejifunza kwa yaliyomtokea na sasa yupo mwangalifu sana na penzi lake, kwani anajua kina dada hawa hawatasita kufanya lolote ili mradi wakuchukulie mpenzi wako na kukuona ukiahangaika. 
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa msanii wa bongo movies kufanya kitendo kama hiki baada ya mwanadada Sintah naye kuamua kumficha mpenzi wake.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top