Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Aunty Ezekiel
Jumatano ya January 14, kwenye XXL ya Clouds FM Soudy Brown amepiga story na muigizaji Aunty Ezekiel kuhusiana taarifa kwamba ni mjamzito na ameonekana akinywa pombe, Soudy alimuuliza kama anafahamu athari za kunywa pombe huku akiwa na ujauzito, Aunty akasema hazijui na yeye sio mjamzito.

PhotoGrid_1420206423320
Soudy alimtafuta pia Dk Makongoro  kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye alielezea kuhusu matatizo ambayo mwanamke anaweza kuyapata iwapo ni mjamzito na anatumia pombe kali, daktari huyo amesema kuwa mama mjamzito anatengeneza mazingiza ya pombe kusafiri kutoka kwake kwenda kwa mtoto na kujitunza kwenye sehemu za ubongo kitendo kinachosababisha mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo  kama mtindio wa Ubongo, Kuzubaa au matatizo ya macho.
Unaweza kuisikiliza U Heard yote hapa.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top