Mhadhiri wa kiislamu siku ya jumamosi amekutwa akiwa amekufa ndani ya gari lake katika mji wa kati wa nchi ya Kenya wa Embu vyanzo vimesema.
Adan Wachu, katibu mkuu wa baraza la waislamu Kenya alisema aliwataarifu Polisi pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la waislamu kuwajulisha tukio hilo.
Mwili huo ulitambuliwa kuwa wa Sheikh Mohamed Ali Kheir ambaye alikamatwa na serikali ya Kenya siku ya Alhamis katika mji wa Mashariki wa Garissa kilomita 400 kutoka Embu ulipokutwa mwili wake Jumamosi.
Mwili huo umekutwa ukiwa na athari ya kupikwa na risasi.
Baadhi ya viongozi wa kiislamu wa Garissa wamesema wahubiri na Masheikh wamekuwa wakikabiliwa na mauaji kwa kisingizio cha kukabiliana na Ugaidi.
Mwaka 2014 wahubiri wanne waliuawa.
Chanzo ahbaabur
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment