Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Penati ya Dakika ya 22 iliyopatika baada ya Mario Gotze kuangushwa ndani ya Boksi na Fernandez na Thomas Muller kufunga, imewapa Bayern Munich ushindi wa Bao 1-0 Ugenini huko Moscow Urusi Katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2014/2015 iliyochezwa Mapema Septemba 30,2014.

 Hii ni Mechi ya Pili ya Kundi E baada ya Bayern kuichapa Man City Bao 1-0 huko Munich.
Kwenye Mechi ya Kundi G la UEFA  iliyochezwa huko Ureno Usiku huu, Jose Mourinho alirudi Nchini kwao na kuiongoza Chelsea kushinda Bao 1-0 walipocheza na Sporting Lisbon.

Bao la Chelsea lilifungwa Dakika ya 34 kwa Kichwa cha Matic ambae ni Mchezaji wa zamani wa Benfica, Mahasimu wa Sporting Lisbon huko Ureno.

MATOKEO.


Jumanne Septemba 30,2014.

KUNDI E

CSKA Moscow 0 – 1 Bayern Munich

Man City 1 – 1 AS  Roma

KUNDI F

APOEL Nicosia 1 – 1  Ajax

Paris St-Germain 3 – 2 FC Barcelona

KUNDI G 

FC Schalke 04 1 – 1  NK Maribor

Sporting Lisbon 0 – 1  Chelsea

KUNDI H 

BATE Borisovs  2 – 1  Athletic Bilbao

Shakhtar Donetsk 2 – 2  FC Porto

Wakicheza kwao Etihad kwenye Mechi ya Kundi E la UEFA, Mabingwa wa Uingereza,  Manchester City, ambao walifungwa Mechi yao ya kwanza 1-0 huko Germany na Bayern Munich, Usiku huu wametoka Sare Bao 1-1 na AS Roma ya Italy.


Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 1-1 kwa City kuongoza Dakika ya 4 tu kwa Penati baada ya Maicon kumwangusha Sergio Aguero na yeye mwenyewe kufunga Penati hiyo lakini katika Dakika ya 23 Francesco Totti, Mkongwe wa Miaka 38, aliisawazishia AS Roma kwa Bao murua.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top