Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Vanessa Mdee aka Vee Money amekanusha tetesi zilizopo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na muimbaji wa ‘Nitasubiri’ Jux.
vanessa
Siku za hivi karibuni, Vanessa na Jux wamekuwa karibu kiasi cha watu kuhisi kuwa ni wapenzi.
“Unajua labda watu hawafahamu tu lakini mie na Jux tumefahamiana muda sana na ni mtu ambaye huwa tunashauriana hasa mambo ya kazi zetu,” amesema Vanessa aliyecheka baada ya kuulizwa swali hilo.


“Ni rafiki yangu wa muda sana sasa hivi. Unajua watu wakikuona upo na mtu karibu tu lazima watasema. Mwanzo walisema Ommy Dimpoz sababu ya ile nyimbo ya Me and You. Mara wakasema Gosby kipindi kile ilipotoka ile nyimbo ya Monefere. Kwahiyo kwahiyo hata leo mfano Nahareel asingekuwa na Aika basi nahisi na yeye pia wangesema hivyo. Ila sio hivyo wanavyofikiria. Jux ni rafiki yangu tu,” Vee ameiambia 
>>>>Bongo5.
Bonyeza Hapa like page yetu

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top