Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MAKOSA ya safu ya ulinzi ya Simba SC, leo yameigharimu timu hiyo kuanza na sare katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Matokeo hayo wazi yatapokewa kwa furaha na wapinzani wa jadi wa Simba SC, Yanga SC ambao jana walianza ligi kwa kichapo cha mabao 2-0 kutoka Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao mawili, yaliyotiwa kimiani na kiungo Shaaban Kisiga ‘Malone’ na mshambuliaji, Amisi Tambwe, lakini baada ya dakika 90 matokeo yakawa 2-2.
Karate, au soka? Kiungo wa Simba SC, Ramadhani SIngano 'Messi' katikati ya wachezaji wa Coastal, Sabri Rashid kulia na Ayoub Yahya katika mchezo wa leo

Mabao yote ya Simba SC inayofundishwa na Mzambia, Patrick Phiri akisaidiwa na wazalendo Suleiman Matola na Iddi Pazi ‘Father’ yalitokana na jitihada za mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Emmanuel Okwi.
Kisiga alifunga bao zuri la kwanza akimtungua Shaaban mwenzake, mtoto wa mzee Hassan Kado kwa mpira wa adhabu dakika ya sita, baada ya Okwi kuangushwa nje kidogo ya boksi.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Miraj Adam, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Pierre Kwizera, Haroun Chanongo/Uhuru Suleiman dk58, Shaaban Kisiga ‘Malone’, Amisi Tambwe/Paul Kiongera dk67/Amri Kiemba dk88, Emmanuel Okwi na Ramadhani Singano ‘

Mabao ya Simba yamefungw na Shaaban Kisiga na Amisi Tambwe

Kikosi cha Coastal Union; Shaaban Kado, Hamad Juma, Sabri Rashid, Abdallah Mfuko, Hamisi Kibacha, Juma Lui, Suleiman Rajab/Yayo Lutimba dk49, Razack Khalfan/Ayoub Athumani dk49, Itubu Imbem, Rama Salim na Joseph Mahundi/Abbas Athumani dk69.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top